Back to top

Bodi ya pamba nchini yapewa siku 3 kumaliza uhaba wa mbegu za pamba.

07 December 2018
Share

Naibu Waziri wa Kilimo Inocent Bashashungwa ameipa siku tatu bodi ya pamba nchini kuhakikisha inamaliza kabisa uhaba wa mbegu za pamba katika mikoa yote inayolima pamba ili kuwaondolea adha wanayoendelea kupata wakulima wa zao hilo.

Naibu waziri huyo ametoa kauli hiyo katika kijiji cha kilalo kilichopo katika wilaya ya bariadi mkoani Simiyu baada ya kupokea malalamiko ya wakulima walimueleza kuhus adha ya upatikanaji wa mbegu.