Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) imeridhishwa na uimarikaji wa umeme katika mkoa wa Mtwara uliyotokana ongezeko la matumizi kutoka Mega Watt 12.5 mwaka 2017 hadi Mega Watt 14 mwaka 2021.
Kauli hiyo ya kuridhishwa ya upatikana ji wa umeme imetolewa na mwenyekiti wa bodi hiyo ya TANESCO Dk. Alexandar Kyaruzi ambao wako Mtwara kutembelea miradi ya umeme na ufanyaji kazi wake.
Amesema uimarikaji wa umeme katika mkoa wa Mtwara unakwenda sambamba na idadi kubwa ya mikoa mingine hapa nchini na kusisitiza kuwa lengo la shirika hilo ni kuona vijiji vyote nchini vinaunganishiwa umeme.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Masasi na Nanyumbu mkoani Mtwara wamesifu serikali kwa juhudi zilizochukuliwa na kufanikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika ambao utachochea wawekezaji mbalimbali katika maeneo hayo.