Back to top

BOKO HARAM WAUA WATU 17 NA KUIBA NG'OMBE KATIKA JIMBO LA BORNO

27 December 2022
Share

Wapiganaji wa kikikundi cha Boko Haram, wamewaua wafugaji 17 na kuiba ng'ombe wao katika Jimbo la Borno, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.

Mapigano yalizuka wakati wapiganaji hao waliposhambulia kundi la wafugaji waliokuwa wakichunga ng'ombe wao kwenye shamba la malisho karibu na kijiji cha Airamne wilayani Mafa.

Kiongozi wa wanamgambo hao Babakura Kolo, amethibitisha kuwa wafugaji 17 wameuawa katika mapigano hayo na ng'ombe wao wote wamechukuliwa.