Back to top

Bondia afariki baada ya damu kuvuja kwenye ubongo.

09 June 2022
Share

Bondia wa Afrika Kusini Simiso Buthelezi amefariki dunia hospitalini kutokana na kuvuja damu kwenye ubongo baada ya kupata jeraha la ubongo wakati wa pambano siku ya Jumapili mjini Durban na Sphesihle Mntungwa.


Katika raundi ya 10, Buthelezi alimsukuma mpinzani wake Mntungwa  kwenye kamba, na wakati anarudi nyuma, Mntungwa alimpiga kwa kishindo kikubwa Buthelezi kidevuni na kuleta athari mbaya kwenye ubongo i na kumfanya apoteze mwelekeo.

Buthelezi alianza kurusha ngumi kupigana na kivuli cha mpinzani asiyeonekana katika upande tofauti na alipo mpinzani wake hali iliyozua sintofahamu na kumfanya muamuzi asimamishe pambano lililopelekea ushindi wa Mutungwa.