Back to top

Benki kuu ya TANZANIA BOT yaiunganisha Twiga Bancorp na TPB.

16 May 2018
Share

Benki kuu ya Tanzani BOT imeamua kuunganisha Benki ya Twiga Bancorp na Benki ya Tanzania Postal Bank Public limited Company TPBPLC.

Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Dokta. Bernard Kibesema amesema benki hiyo ya Twiga Bancorp iliyokuwa chini ya usimamizi wa benki kuu kwa sasa imeunganishwa na benki ya posta na kwamba utekelezaji wa hatua hiyo unaanza mara moja Mei 17 mwaka huu ambapo mali za wateja na madeni ya benki hiyo sasa yatasimamiwa na benki ya Tanzania Postal Bank Public Limited Company.

Dokta Kabesema amesema baada ya kuuganishwa huko anategemea kutakuwa na ufanisi mkubwa katika utendaji kwa wateja wa benki hiyo.

Kwa upande wake meneja uendeshaji wa bodi ya bima ya amana Bi Rosemery Tenga amewataka walikuwa wateja katika benki ambazo zipo chini ya BOT kufuati mitaji ya benki hiyo kuyumba kwenda katika benki hizo na utaratibu wa malipo utafanyika chini ya usimamizi wa bodi ya amana.