Back to top

KITENGO CHA MAWASILIANO MNH CHAPONGEZWA

11 June 2025
Share

Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga na Mloganzila umeipongeza Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano cha hospitali hiyo kwa kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kuitangaza vema hospitali hiyo ndani na nje ya nchi.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo, Prof. Mohamed Janabi wakati wa Mkutano wa 30 Baraza la Wafanyakazi linalofanyika katika ukumbi wa PSSSF mkoani Dar es Salaam.

Prof. Janabi ameongeza kuwa kutokana na utendaji kazi wa kitengo hicho jamii imeweza kufahamu huduma mbalimbali zinazotolewa na hospitali hiyo na kuifanya jamii kuwa na taarifa za kutosha na uhakika hivyo kuwafanya kunufaika na uwekezaji ulifanywa na serikali yao.

“Kwa niaba ya Menejimenti nawapongeza sana kwa kazi mnayoifanya, hakuna ubishi mmefanya kazi kubwa sana, mmeifanya hospitali yetu kuendelea kuwa kiongozi na kuwa mfano wa kuigwa nchini na Afrika Mashariki na Kati katika utoaji wa huduma za afya.

Akipokea pongezi hizo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano MNH, Bw. Aminiel Aligaesha amesema pongeza hizo zimeendelea kuwa chachu ya uwajibikaji kwa watumishi wa kitengo hicho na kuahidi wataendelea kutekeleza majukumu kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo.