Back to top

BreakingNews:Masauni aagiza kusimamishwa kazi askari wanne wa Magereza

22 March 2019
Share

Naibu Waziri wa mambo ya ndani Mhe.Hamad Masauni amemuagiza Kamishna Jenerali wa Magereza kuwasimamisha kazi askari wanne wa jeshi la Magereza katika Gereza kuu la Luanda jijini Mbeya baada ya kuwakuta wafungwa wakiwa na dawa za kulevya na simu za mkononi Gerezani.

Mh.Masauni amesema kuwa amekamata simu 10 kutoka kwa wafungwa na kuzikabidhi kwa jeshi la polisi kisha kufanyiwa uchunguzi, ambapo imebainika kuwa simu hizo zinatumika kufanya uhalifu, ikiwemo vitendo vya rushwa ambapo kuna baadhi ya miamala ya kifedha inafanywa baina ya wafungwa/ ndugu na baadhi ya askari Magereza katika gereza kuu la Luanda.

Amesema aina ya dawa za kulevya alizozikuta kwa wafungwa hao ni bangi, ambapo wafungwa wamekuwa wakivuta bangi wakiwa gerezani huku pia wakiwa wamehifadhi bangi ndani ya gereza jambo alilosema ni kinyume kabisa na utaratibu wa uendeshaji wa gereza na kinyume cha sheria za nchi.

Kufahamu zaidi Bonyeza Video hiyo hapo chini.