Back to top

Bugando kwa mara ya kwanza yafanya upasuaji wa nyonga na magoti.

09 July 2020
Share

Hospitali ya Rufaa ya kanda Bugando jijini Mwanza kwa mara ya kwanza imeendesha kambi ya huduma za upasuaji wa nyonga na magoti ambazo hazikuwahi kutolewa katika hospitali hiyo tangu kuanzishwa kwake, ambapo wagonjwa 10 kati ya 300 waliojitokeza kupata huduma hiyo katika muda wa siku tano watafanyiwa upasuaji na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Mifupa (MOI).

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo Dk. Fabian Masaga anasema kambi hiyo maalum kwa ajili ya upasuaji wa nyonga na magoti iliyoanza Juni 6 hadi Juni 10 mwaka huu imeandika historia baada ya zaidi ya wagonjwa 300 kujitokeza kufanyiwa uchunguzi ambapo wagonjwa watano tayari wamefanyiwa upasuaji huo.