Back to top

Bunge la Ulaya la hofia Corona, kufanya vikao yake kwa njia ya simu

28 February 2020
Share

Bunge la Ulaya linazingatia kuhusu iwapo linaweza kufanya mikutano na vikao vyake vya awali kwa njia ya simu.

Hiyo inatokana na kuongezeka kwa wasiwasi kuhusu maradhi ya virusi vya Corona yanayosambaa kwa kasi duniani.

Msemaji wa bunge hilo amesema wanaliangazia kwa kina suala hilo na kuahidi kutoa ufafanuzi kamili siku chache zijazo.

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema, hakuna nchi inayopaswa kudhani kwamba haitaathiriwa na virusi hivyo vya Corona.

Serikali mbalimbali duniani ikiwemo ya Iran hadi Australia zinapambana kuhakikisha wanafanikwia kuzuia kusambaa zaidi kwa janga hilo.