Bunge limeagiza kuwa wizara zote ambazo sheria zake zimeonekana kuwa na dosari katika utelezaji wake kupitia majedwali yaliyopitishwa na bunge hilo zifanyiwe marekebisho ili kuondoa dosari hizo ili malengo yaliyokuwa yamekusudiwa yaweze kutimia.
Akiwasilisha taarifa ya kamati ndogo kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo zilizowasilishwa katika mkutano wa kumi na moja wa bunge Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh.Andrew Chenge amesema marekebisho hayo yatasaidia sheria hizo kutumiwa vyema.
Awali kabla ya bunge kufanya mazimio hayo baadhi ya wabunge walipata wasaa wa kuchambua marekebisho hayo.
Aidha katika kikao hicho Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage alitoa Bungeni taarifa ya sukari kuhusu upatikanaji wake na sababau za bei ya sukari kupanda.
Kufuatia taarifa hiyo baadhi ya wabunge walitoa maoni yao na kusema kuna haja ya serikali kuona ni hatua gani za kufanya ili kuhakisha bei ya sukari inashuka sambamba na kuhakisha upatikanaji wake unakuwa wa uhakika.