
Rais wa mpito wa Burkina Faso, Ibrahim Traoré amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Urusi Yunus-bek Yevkurov.
.
Mazungumzo hayo yamedaiwa kulenga zaidi masuala ya usaidizi wa kijeshi ikiwa ni pamoja na mafunzo kwa maafisa na marubani wa Jeshi la Burkina Faso.
.
Ziara hiyo iliyoongozwa na Waziri Yunus-bek, ni moja wa ufuatiliaji wa mazungumzo yaliyofanyika kati ya Rais Traoré na Rais Vladimir Putin katika mkutano wa Viongozi wa Afrika na Urusi uliofanyika St Petersburg, nchini Urusi.
