Back to top

"BUSARA ITUMIKE KUTATUA CHANGAMOTO, SEKTA YA ARDHI"

11 March 2024
Share

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe, Geophrey Pinda, amewataka watumishi wa sekta ya ardhi nchini kutumia busara wakati wote wa kushughulikia changamoto za sekta ya ardhi.

Mhe.Pinda ametoa kauli hiyo, wakati wa uzinduzi wa Kliniki ya Ardhi katika mkoa wa Mwanza, na kubainisha kwamba watendaji wa sekta ya ardhi wasiposimamia katika kuwatafutia haki wananchi watasababisha malalamiko yasiyo na tija.

Mhe.amewaasa watendaji wa ardhi kufuata sheria na kuwa na maadili mema wakati wote wa kutekeleza majukumu yao pamoja na kujiepusha kabisa vitendo vya rushwa.

 

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi ameitaka Ofisi ya Aradhi mkoa wa Mwanza kuhakikisha inaharakisha utoaji hati milki za ardhi na kuongeza kuwa wizara yake haitasita kumchukulia hatua mtumishi yeyote atakayekwamisha kazi hiyo.

Kwa mujibu wa Mhe, Pinda, Wizara ya Ardhi inakamilisha Maboresho ya mfumo wa TEHAMA utakaoruhusu huduma na miamala ya sekta ya ardhi kutolewa kidigitali. Mfumo huo utaanza kutumika hivi karibuni kwa kuanza na mikoa ya Arusha, Tanga, Mwanza na Mbeya.

Amempongeza Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuiwezesha Wizara yetu kufanikisha miradi mbalimbali inayoenda kuondoa changomoto katika sekta ya ardhi. Hakika huyu ni Mama wa kipekee na Mungu ampe maisha marefu.

Akielezea zaidi kuhusu Klinik aliyoizindua, Naibu Waziri wa Ardhi amesema uzinduzi wa Kilink hiyo ni  muendeleo wa Kliniki za Ardhi zilizofanyika maeneo mbalimbali nchini hususan katika majiji makubwa kama vile Dar es Salaam na Dodoma.