Back to top

Jicho la CAG labaini KMC kudaiwa mkopo milioni 33 malipo ya kocha.

08 April 2021
Share


Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG Charles Kichere katika ripoti yake kwenye Manispaa ya Kinondoni Mkoani Dar es salaam imebaini kuwa kiasi cha shilingi milioni 33 zilizotolewa na Halmashauri hiyo katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2019/20 kama mkopo wa mshahara kwa mwalimu wa timu ya KMC hakijarudishwa.


"Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20 Halmashauri ilimpatia mkopo wa mshahara (Advance salary) kiasi cha shilingi mil 33 mwalimu wa timu ya mpira wa miguu inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni yaani Kinondoni Municipal Council Football Club kupitia hundi namba 368 ya tarehe 21 June 2019, mpaka ukaguzi huu unakamilika mwezi Agosti mkopo huu ulikuwa bado kurejeshwa, na sina hakika kama mwalimu huyu bado yupo pale". Alisema CAG Kichere.