Back to top

CCM kuigawa wilaya ya Bagamoyo na kuunda wilaya mpya ya Chalinze.

19 October 2020
Share

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM Dk.John Magufuli amewaomba wakazi wa mkoa wa Pwani waichague CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao ili ikamilishe mradi mikubwa wa maji kutoka mto Ruvu na kuboresha mazingira ya wavuvi wadogo kwenye fukwe za bahari ya hindi katika mkoa wa Pwani.

Dkt.John magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM ameyasema hayo wakati akizungumza maelfu ya wakazi wa wilaya ya Bagamoyo kwenye mkutano wa kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kwenye uchaguzi mkuu.
 
Amesema endapo atapata ridhaa ya kurejea tena madarakani serikali yake itaigawa wilaya ya Bagamoyo na kuunda wilaya mpya ya Chalinze hili kusogeza huduma karibu na wananchi pamoja na kuboresha mazingira ya wavuvi katika fukwe za bahari ya hindi .

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Mwenyekiti mstaafu na Rais wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete ambaye pia alitoa neno kwa kuhusu ushindi wa chama cha Mapinduzi.