Back to top

CCM yalaani mauaji ya baadhi ya wafuasi wa chama hicho.

17 October 2020
Share

Chama cha Mapinduzi CCM kimelaani vikali mauaji ya baadhi ya wanachama wake yaliyotokea katika maeneo mbalimbali nchini na kusababisha wananchi wengine kujeruhiwa yanoyodaiwa kufanywa na baadhi ya watu kwa lengo la kuvuruga amani nchini huku wanachama wakiombwa kutolipiza kisasi.

Hayo yamebainishwa na katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi wa CCM Dkt.Bashiru Ally wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho na mawakala wa uchaguzi wa chama hicho wa wilaya ya Nyamagana katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Katika hatua nyinginge Dkt.Bashiru amewataka mawakala wa uchaguzi wa chama hicho kufanya kazi kwa uadilifu na kulinda maslahi ya chama kwenye vituo vya uchaguzi.