Back to top

CCM:Rais Samia apitishwa kuwa mgombea pekee nafasi ya Mwenyekiti Taifa

29 April 2021
Share

Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa kwa kauli moja imepitisha azimio la kupitisha jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea pekee wa nafasi ya mwenyekiti taifa wa chama hicho katika mkutano mkuu maalum utakaofanyika jijini Dodoma Apriil 30, mwaka huu.

Viongozi na Wajumbe mbalimbali wa NEC akiwemo Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan wakiwa katika Kikao cha NEC kilichofanyika tarehe 29 Aprili, 2021.


Akizungumza jijini Dodoma mara baada ya kikao cha Halmashauri kuu ya chama hicho kupitisha jina la Mhe.Rais Samia kugombeaa nafasi hiyo katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho Bw.Humprey Polepole amesema katika kikao hicho wajumbe wote kwa kauli moja wameunga mkono kupitishwa kwa azimio hilo na kupeleka jina la Mhe.Rais Samia katika mkutano mkuu maalum.
.
Katika hatua nyingine Bw.Polepole amesema pamoja na agenda ya azimio la kupitisha jina Mhe.Rais Samia wajumbe wa mkutano maalum watakuwa na kazi ya kupitisha majina yaliyochaguliwa na Halmashauri Kuu kwa ajili ya kujaza nafasi mbalimbali za viongozi zilizo wazi kuanzia ngazi ya taifa mkoa hadi wilaya.

.
Aidha, Wakati huo jiji la Dodoma limezidi kufurika idadi ya watu kufuatia ujio wa wajumbe wa mkutano huo.