Back to top

CHADEMA kutoshiriki uchaguzi serikali za mitaa kwamuibua Jafo.

07 November 2019
Share

Muda mchache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kutoa tamko la kutokushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Waziri Waziri Ofisi ya rais TAMISEMI Seleman Jafo amesema kitendo cha viongozi wakuu wa CHADEMA kutangaza kutoshiriki uchaguzi ni kuwanyima haki ya msingi watu wengine ambao majina yao yalishateuliwa.


"Muda wa kukata rufaa umefika na watu wengine fomu wanakosea kujibu kwa makusudi, Je ulikuwa mpango mkakati wa kuwaelekeza fomu ziharibike ili kujitoa kwenye uchaguzi, kwa hiyo ni maswali ambayo nakosa kupata majibu,  mimi kwa imani yangu nadhani kwamba inawezekana wanawanyima haki ya msingi huku chini watu wengine ambao majina yao yashateuliwa, watu wengine wamekata rufaa na rufaa zao kesho zinatoka leo hii viongozi wakuu wanatangaza kujitoa katika uchaguzi"-Selemani Jafo -Waziri TAMISEMI.