Back to top

CHADEMA waitaka NEC kutaja kampuni inayochapisha karatasi za kura.

10 October 2020
Share

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuitaja kampuni iliyopewa tenda  ya kuchapisha karatasi za kupigia kura na kueleza umma wazi mchakato wa manunuzi ulivyopitiwa kutokana na uwepo wa tetesi za taasisi mbili zinazotajwa kupewa zabuni hiyo huku wakiwa na walakini na moja ya kampuni tajwa. 


Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Makao Makuu ya chama hicho Katibu Mkuu wa chama hicho John Mnyika amesema licha ya tume kuitisha kikao cha kwanza tarehe nane mwezi Oktoba hata kamati ya zabuni na manunuzi inayohusisha vyama vya siasa aijaelezwa jina la kampuni iliyopewa zabuni licha ya uwepo wa majina mawili ambayo yametajwa.

Aidha Mnyika ameitaka tume kuweka wazi mfumo wa ujumlishaji wa matokeo ya uchaguzi huku akisema wamepeleka malalamiko kwa tume baada ya mgombea wa CCM kukiuka taratibu za kiuchaguzi na kufanya kampeni yake binafsi na wagombea wengine katika kazi ya serikali wakati wa uzinduzi wa stendi ya mabasi Mbezi.

Wakati huo huo Mnyika amemtaka IGP Simon Sirro kumchukulia hatua OCD wa Hai na si kuanza masuala ya kutaka  kuunda kamati ya kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa chama hicho na mgombea wa jimbo la Hai Freeman Mbowe  kwa kumtamkia mgombea huyo kuwa hatashinda uchaguzi.