Back to top

CHADEMA yasusia uchaguzi serikali za mitaa.

07 November 2019
Share

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimejitoa kushiriki uchaguzi wa serikali kwa madai kuwa zoezi hilo limegubikwa na ukiukwaji mkubwa wa demokrasia huku Mwenyekiti wake Freeman Mbowe akisema asilimia 85 ya wagombea wa chama hicho nchi nzima majina yao yametolewa kwa hila na kubaki asilimia 9 tu.


Maamuzi ya kujitoa kwenye kushiriki uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu umetokana na vikao vya kamati kuu na halmashauri kuu ya chama hicho vilivyofanyika Dodoma.