Back to top

CHAKUA yatoa namba kwa abiria kuwabana madereva.

15 October 2018
Share

Chama cha kutetea abiria CHAKUA kimetoa namba 0719 27 79 01 kwa abiria ili waweze kuwapigia pindi dereva anapoingiza gari kwenye kituo cha mafuta likiwa na abiria.

Akiongea na Radio One kupitia kipindi cha Kumepambazuka Mwenyekiti wa CHAKUA Bw.Hassan Mchanjama amesema lengo la kutoa namba hiyo ni kuhakikisha usalama wa abiria unalindwa muda wote na hasa kwenye vituo vya mafuta.

Bwana Mchanjama amesema maofisa wa chama hicho kwa sasa wametapakaa nchi nzima kwa lengo la kufuatilia magari yanayojaza mafuta yakiwa yamebeba abiria, huku akiitaka EWURA izibane Petrol Station (vituo vya mafuta) kutoa huduma kwa mabasi yaliyobeba abiria na kuingia vituoni humo ili kuepusha majanga ambayo yanaweza kuzuilika kwani ni kinyume cha sheria za Sumatra, Trafic na EWURA.

Kwa upande wake Afisa Mipango kutoka RSA Bi.Irene Mselemu amesema ili kuhakikisha zoezi hilo linaleta matokeo mazuri nivema jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kuhakikisha kwamba linawaelekeza askari wake kukabiliana na baadhi ya mabasi yatakayokuwa yakiingia kujaza mafuta kwenye vituo vya mafuta yakiwa na abiria.

Ameongeza kwa kusema kuwa endapo nguvu itaelekezwa huko kama ilivyoelekezwa katika maeneo mengine ni dhahiri kwamba usalama wa abiria utakuwa ni mkubwa anapokuwa katika safari kutoka eneo moja mpaka lingine.