
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe.Damas Ndumbaro amesema kuhusu suala la Katiba, watu wengi wanaweka mbele mahitaji ya kisiasa na kusahau kuwa kwenye katiba, kuna mahitaji mengine, zaidi ya siasa.
.
Ndumbaro ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari , baada ya Mjadala wa Katiba mpya, kuelekea mkakati wa Taifa wa elimu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa umma, ulioendeshwa na Wizara hiyo.
.
Mjadala huo umewahusisha Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu wastaafu na waliopo ambao wamesisitiza uhitaji wa kupewa kipaumbele kwa mchakato mzima wa Katiba, na kuhakikisha hawafanyi makosa yaliyofanyika nyuma.
