Back to top

Changamoto ya zahanati kuwa na mtumishi mmoja yatatuliwa Tunduru.

01 July 2020
Share

Siku chache baada ya ITV kuripoti  zahanati ya kijjiji cha Kajima kata ya Jakika wilayani Tunduru mkoani Ruvuma  kuwa  na mtumishi mmoja  ambaye  akiwa na dharura inafungwa na wananchi wanakosa huduma za matibabu serikali  imeongeza mtumishi mmoja kwenye zahanati  hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Bw. Gaspar Balyomi amesema kuwa hategemei kuona wananchi wakikosa huduma za matibabu katika kijiji hicho kwa zahanati kufungwa kwa kuwa kwa sasa watakuwa wakipokezana pindi mmoja anapokuwa na dharura.