Back to top

"CHANGAMOTO ZA MUUNGANO ZINATAFUTIWA UFUMBUZI" - MWINYI

14 April 2024
Share

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, amesema ni wajibu kuulinda, kuuendeleza, kuudumisha na kuimarisha zaidi Muungano, ili kuzidi kunufaika kwa dhamira ile ile ya Waasisi wa Taifa letu.
.
Rais Mwinyi amesema hayo, leo Aprili 12, 2024, wakati akifungua  Maadhimisho ya Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaliyoambatana na Maonesho ya Taasisi mbalimbali, katika viwanja vya Nyamanzi, vilivyopo mkoani Mjini Magharibi, ambapo pia ameeleza kuwa umoja na ushirikiano wa Watanzania unazidi kuimarika, katika shughuli mbalimbali na amani inaendelea kudumu nchini.
.
Aidha Rais huyo amesema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zinaendelea kuchukua hatua madhubuti za kuzitafutia ufumbuzi changamoto zote zinazojitokeza katika utekelezaji wa masuala ya Muungano ambapo katika kipindi cha miaka mitatu, 2021 hadi mwaka 2024 hoja 15 zimepatiwa ufumbuzi kati ya hoja 18 zilizokuwepo.
.
Pia,Rais Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka vipaumbele masuala ya kuimarisha Muungano huku akieleza kuwa Tanzania imefikia mafanikio makubwa kipindi cha  Miaka 60 katika nyanja zote za maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na huduma za jamii.