Back to top

Chanzo cha ndege za Kenya kuzuiwa kutua nchini.

01 August 2020
Share

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania  TCAA imefuta kibali kilichokuwa kikiruhusu  ndege za Shirika la ndege la Kenya kutua Tanzania.

Akizungumza na katika mahojiano maalum Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Hamza Johari amesema uamuzi huo umekuja baada Kenya kutoijumuisha Tanzania katika orodha  ya nchi ambazo raia wake wataruhusiwa  kuingia Kenya.

Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi nchini Kenya James Macharia amesema kuwa wamepokea taarifa hiyo kutoka Serikali ya Tanzania huku akikanusha taarifa ya ndege za Tanzania kuzuiwa kuingia nchini Kenya na kueleza kuwa waliamua ndenge za Tanzania zinapoingia Kenya abiria wake wangetakiwa kukaa karantini ndani ya siku 14.

Naye Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania mhandisi Isack Kamwele amesema kutakuwa na kikao siku ya Jumanne kilichoitishwa na Wizara ya Mambo ya Nje ili kujadili suala hilo.