Back to top

Chatu anayeshambulia binadamu na wanyama azua Taharuki, Songea.

22 March 2018
Share

Wananchi wa kata ya Mshangano manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wameingiwa na hofu na taharuki kutokana na chatu ambaye  amekuwa akishambulia wanyama na binadamu na kusababisha shughuli za maendeleo kusimama ambapo wananchi wanahisi nyoka  wamevunja kwenye wigo wa hifadhi ya wanyamapori na kuingia mitaani.

Wananchi wa mtaa wa Namanyigu kata ya Mshangano wanaitisha kikao cha dharura kujadili tatizo la chatu anayewasumbua  kwa zaidi ya wiki mbili anavyowasumbua ambapo kijana aliyenusurika kumezwa na chatu anaeleza namna alivyoweza kujinasua  kutoka kwa chatu anayewasumbua.

Licha ya chatu wananchi pia wanasema kuwa kuna nyoka wengine wanaosumbua wananchi wakiwakimbiza na hivyo wanahisi wamevunja wigo wa bustani ya wanyamapori ya Luhira na kuingia mitaani.

Kutokana na hali hiyo askari wa wanyamapori wanaingia katika pori la namanyigu kufanya msako dhidi ya chatu huyo na pia wanaenda kutoa  elimu kwa wanafunzi katika shule ya msingi Luhira mchanganyiko ili kuwalinda wanafunzi dhidi ya chatu hata hivyo hawakufanikiwa kumuona chatu huyo.