Back to top

CHAUMA chatangaza kutoshiriki uchaguzi Serikali za Mitaa.

09 November 2019
Share

Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), kimejiondoa katika kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa madai kuwa wagombea wake zaidi ya 250 wa chama hicho wameenguliwa bila sababu.

Mwenyekiti wa chama hicho, Hashim Rungwe amesema inashangaza kuona wapinzani tu ndio wanaokosea kujaza fomu katika mchakato huo, hivyo wameona nibora wakae pembeni.

Chama cha Chauma kinakuwa chama cha Tatu sasa kususia uchaguzi serikali za Mitaa baada ya CHADEMA na ACT Wazalendo kujiondoa kwenye mchakato huo, huku visa vikionesha kufanana katika mchakato huo, ambapo uchaguzi huo wa Serikali za mitaa unatazamiwa kufanyika 24 Novemba 2019.