
Wanafunzi watatu wakiume wenye umri chini ya miaka 14 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini China, kufuatia kifo cha kikatili cha mwenzao (13) aliyefahamika kwa jina moja la ukoo la wang ambaye mabaki ya mwili wake yamekutwa yamezikwa katika bustani ya mboga iliyotelekezwa.
Kwa mujibu wa baba wa mtoto huyo anasema kabla ya kifo cha mtoto wake alihamisha yuan 191 ($17; £13) kwa mmoja wa wanafunzi wenzake watatu, baba huyo aliambia The Beijing News.
"Alikuwa ameonewa na wanafunzi wenzake hao watatu kwa muda mrefu".Wakili wa familia hiyo, Zang Fanqing.
Polisi wanachunguza kesi hiyo kama mauaji ya kukusudia. Kesi ya mvulana huyo imezua hasira na mjadala mkali kuhusu uhalifu wa watoto.
Vijana wote watatu wanaozuiliwa wako chini ya umri wa miaka 14. Chini ya sheria ya China, wale walio na umri wa zaidi ya miaka 12 lakini walio chini ya miaka 14 wanaweza kukabiliwa na mashtaka ya jinai tu wanaporuhusiwa na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Umma, mwendesha mashtaka mkuu zaidi wa nch
Wakihojiwa na mamlaka, wavulana hao watatu waliwaongoza polisi hadi kwenye mwili wa mvulana huyo, baada ya awali kukanusha kuwa hawajui ulipozikwa.
