Back to top

China yatoa msaada wa Bilioni 146.4 kwa serikali ya Tanzania.

19 May 2018
Share

Serikali ya Tanzania imesaini makubaliano ya msaada wa zaidi ya Shilingi Bilioni 146.4 na Serikali ya Jamhuri wa watu wa China kwa ajili ya ujenzi wa chuo kikuu cha usafirishaji pamoja na ujenzi wa reli ya kati ya kisasa ili kusaidia kusukuma maendeleo.

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, Katibu Kkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bwana Doto James amesema katika fedha hizo dola Bilioni 62 zimetolewa msaada kwa ajili ya ujenzi wa chuo kikuu cha taifa cha usafirishaji huku kiasi kilichobaki kitatumika kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa reli ya kati ya kisasa.

Balozi wa China hapa nchini Bi. Wang Ke amesema serikali ya China imejipanga kuzisaidia nchi tano za Afrika katika sekta ya usafirishaji kwenye maeneo matatu ikiwemo, Miundombinu, usafirishaji pamoja na utaalamu ambapo kwa upande wa Tanzania tayari imeanza na msaada wa ujenzi wa chuo kikuu cha usafirishaji pamoja na reli ya kisasa.

Kwa upande wake mkuu wa chuo cha usafirishaji Profesa Zacharia Mganiliwa amesema ujenzi wa chuo kikuu hicho utasaidia kupatikana wataalamu katika sekta mbalimbali watakaosaidia katika miradi mbalimbali ya serikali ikiwemo maboresho katika sekta ya usafirishaji wa anga na reli, huku Kaimu Mkurugenzi wa reli Bwana Foxcusd Makoye amepongeza serikali ya awamu ya tano kwa kutoa kipaumbele katika sekta ya usafirishaji.