Back to top

CHINA YATOA MSAADA WA MAGARI 8 KWA EAC

27 June 2023
Share

Serikali ya China imetoa msaada wa magari 8, wenye thamani ya Dola laki nne za kimarekani, kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), unaolenga kuiwezesha jumuiya hiyo kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.

Akikabidhi magari hayo Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian, amesema msaada huo ni muendelezo wa ushirikiano baina ya nchi ya China na Jumuiya ya Afrika Mashariki.