Back to top

Clatous Chama hang'ooki Simba Ng'o...,Simba yasema inamkataba naye.

11 August 2020
Share

Ungozi wa Simba umesema kuwa suala la mchezaji wao Clatous Chama kutajwa kujiunga na watani zao wa jadi Yanga hazina ukweli.

Imekuwa ikiripotiwa kuwa baada ya Yanga kumchukua aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mbatha imeanza hesabu za kumvuta ndani ya kikosi kiungo wao bora, Chama.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Simba haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo kwa kuwa ina mkataba naye na ina malengo.