Back to top

Corona Kenya yapamba moto, Vyuo vikuu kufunguliwa 2021.

30 July 2020
Share

Waziri wa Elimu nchini Kenya Prof.George Magoha ametangaza kutofunguliwa kwa Vyuo Vikuu  nchini humo mwaka huu kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona.

Waziri Magoha amesema vyuo hivyo vilipangwa kufunguliwa Septemba mwaka huu hivyo havitafunguliwa tena badala yake vitafunguliwa tena Januari 2021 kama ilivyo kwa shule za Msingi na Sekondari nchini humo.

Wakati tamko hilo la kutokufunguliwa kwa vyuo likiwa limetolewa maambukizi ya Covid -19 mpaka sasa yamefikia 19,125.