Back to top

'CORONA' Shirika la Afya Duniani (WHO) lakubali kuchunguzwa.

20 May 2020
Share

Shirika la Afya Duniani limekubali kuanzisha uchunguzi ufanywe dhidi yake kuhusu namna lilivyoushughulikia mzozo wa virusi vya corona, kati yake, Marekani na China baada ya rais Donald Trump kutishia kujiengua kwenye shirika hilo.

Mkurugenzi Mkuu shirika hilo Dakta Tedros Adhanom Gebreyuses amesema mapambano ya janga hilo ni lazima yapewe kipaumbele, ingawa maradhi ya COVID-19 yanaendelea kusababisha vifo na kudhoofisha chumi kote ulimwenguni.

Rais Trump amelituhumu Shirika la Afya Duniani kwa kuwa  kibaraka wa China na limeshindwa kufanya vya kutosha kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Jumatatu iliyopita Rais Trump alitishia kuondoa kwa muda ama moja kwa moja ufadhili wa Marekani kwenye shirika hilo, tishio ambalo China ililijibu kwa kumtuhumu Rais Trump kwa kujaribu kuichafua China na kulivuruga Shirika la Afya Duniani kwa manufaa ya kisiasa.