China imetoa taarifa mpya kuhusiana na ugonjwa wa Virusi vya Corona ambapo vifo zaidi ya 121 vimeripotiwa kati ya hivyo vifo 116 vikitokea katika mjiwa Hubei pekee.
Tume ya afya nchini humo imesema kuwa mpaka sasa vifo vilivyotokana na ugonjwa huo nchini humo vimefikia 1,384
Leo Ijumaa kuna taarifa mpya 64,456 za maambukizi mapya ya ugonjwa huo wa virusi vya Corona, huku wanaoendelea kuimarika afya zao wakifikia 7,101
Nayo nchi ya Vietnam imeamuru kufungwa mji mkuu Hanoi, na kuwa eneo la kwanza nje ya Uchina kuwekwa chini ya karantini kwa siku 20.