Back to top

Corona yasababisha serikali kushindwa kuongeza viwango vya mishahara.

01 May 2021
Share

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaondoa hofu wafanyakazi kote nchini kwa kushindwa kuongeza viwango vya mishahara katika bajeti ya mwaka huu kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona kuathiri uchumi na badala yake amepunguza kodi katika mishahara na kufuta baadhi ya tozo katika stahiki zingine za wafanyakazi na kuahidi kuongeza mishara hiyo bajeti ijayo.


Akizungumza na mamia ya watanzania kutoka maeneo mbalimbali nchini waliohudhuria maadhimisho hayo ya Mei Mosi katika uwanja wa Ccm Kirumba Jijini Mwanza, Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema anatambua changamoto zinazowakabili wafanyakazi wenzake na ameagiza kuundwa kwa bodi ya mishahara ili iiweze kumsaidia katika mpango wa kuongeza mishahara katika bajeti ya mwaka wa fedha 21/22.


Akiwawakilisha wafanyakazi nchini Rais wa Shirikisho la Wafanyakazi (TUCTA) Tumaini Nyamhokya amemuomba Rais kuliangalia suala la kupandishwa madaraja kwa watumishi  na malimbikizo ya madeni ya wafanyakazi yanalipwa kwa spidi ndogo.


Aidha rais samia ametangaza rasmi kuongezwa kwa umri wa wategemezi wa bima za afya kutoka 18 ya awali hadi miaka 21 kwani bado wanakua ni tegemezi.