Back to top

CRDB kutoa elimu ya mirathi na wosia kwa wateja wake.

17 April 2018
Share

Benki ya CRDB tawi la Shinyanga imeanza mpango maalum wa kutoa elimu ya mirathi na wosia kwa wateja wake, lengo likiwa ni kuwawezesha kutambua umuhimu wa kuandika na kuacha wosia.

Mpango huo una tarajiwa kupunguza matatizo kufuatilia mali za wateja wa benki hiyo pale wanapofariki dunia.

Kaimu Meneja Mkuu wa CRDB tawi la Shinyanga, Bi.FORTUNATA MPARA amesema benki imefikia uamuzi wa kutoa elimu ya mirathi na wosia kwa wanahisa na wateja ili wajue kuwa hisa ni mali kama mali nyingine zinazostahili kurithiwa endapo mmiliki atafariki dunia.

Kwa upande wake Afisa wa Sheria katika Benki ya CRDB nchini, Bwana. MARIJANI KIZIGA amesema elimu hiyo inatolewa ili kuwasaidia wahusika wajue taratibu za kufuata endapo litatokea jambo linalohusiana na mirathi kwa mwanahisa au mteja wa benki hiyo.