
Dada wa Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, Bi. Yo-Jong ametoa onyo kwa Korea Kusini kuwa endapo nchi hiyo itaishambulia Korea Kaskazini, wataishambulia nchi hiyo kwa makombora ya nyuklia.
.
Kauli hiyo ya Bi. Yo-Jong inafuata baada ya Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini kusema kuwa Jeshi lake lina uwezo wa kushambulia eneo lolote ndani ya Korea Kaskazini.
.
Hata hivyo, Korea kaskazini imesema haitaki vita kwa hivyo haitakuwa ya kwanza kushambulia.
