Back to top

Dada wa Ronaldo amtolea uvivu Vigil Van Djik kwa kumdhihaki kaka yake

03 December 2019
Share

Dada yake na Cristiano Ronaldo, Katia aveiro amemchana beki wa Liverpool Vigil Van Djik kwa kumdhihaki kaka yake kwenye tuzo za Ballon Dor.

Katika tuzo hizo Vigil Van Djik ambaye alishika nafasi ya pili alivyoulizwa kuhusu Cristiano Ronaldo ambaye hakuwepo wakati wa Messi akiichukua kwa mara ya 6 alisema kwa utani kuwa "kwani Ronaldo naye alikuwa anawania?" yani kana kwamba Ronaldo sio wa kiwango cha tuzo hiyo.

Lakini licha ya kitu alichosema hakumaanisha kwakuwa alikuwa anatania, dada wa Cristiano Ronaldo Katia Aveiro ambaye pia ni mwanamuziki amemshushia maneno kuntu Vgil Van Djik kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa asijilinganishe yeye na Ronaldo kwakuwa huko alipo Ronaldo aliishagang'ara kitambo. 

"Mpendwa Vigil Cristiano Ronaldo aling'aa kwenye ligi unayocheza na alienda kwenye klabu nyingine ya Real Madrid nako akawa mchezaji mkubwa kwenye historia ya klabu hiyo, nikwambie kitu Vigil au kwasababu klabu hiyo ikiwa na huyu Cristiano Ronaldo iliwafunga kwenye mchezao fainali ya UEFA Champions League" alisema Katia Aveiro.