
Mahakama ya Wilaya Kigamboni imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 40 jela mtuhumiwa Daniel Shirwa Mandele mwenye umri wa miaka 35, mjasiriamali, mkazi wa Kibada Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam baada ya kupatikana na hatia ya kosa la shambulio la aibu kwa kuwawekea vidole sehemu za siri na kuwatolea uume wake wachezee watoto wawili wa kike mmoja mwenye umri wa miaka 4 na mwengine miaka 5 wanafunzi wa chekechea wakazi wa Kibada ambao ni watoto wa wapangaji wenzake.
Imeelezwa kuwa mnamo Juni 20, 2025, majira ya saa 08:00 mchana huko Kibada, mtuhumiwa aliwaita watoto hao chumbani kwake wakati wazazi wao wakiwa wametoka na kisha kuwapa simu ili waangalie katuni na kuanza kuwaingizia vidole sehemu za siri na kisha kutoa maumbile yake ya siri na kuwashikisha watoto hao na baadae kuwarubuni kwa pipi na biskuti ili wasiseme kwa wazazi wao.
Akisoma hukumu hiyo Februari 05, 2026, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya Kigamboni Mhe. Baro ameeleza kuwa ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo pasi na chembe ya shaka umeweza kumuunganisha mtuhumiwa kutenda kosa hilo hivyo ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.
