Back to top

DAR: BEI YA PETROLI YAPANDA KUTOKA 3,163/= HADI 3,257/=

03 April 2024
Share

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya za mafuta hapa nchini, zitakazoanza kutumika leo Aprili 03, 2024, ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, mafuta ya petroli ni Tsh.3,257/= yakiwa yamepanda kutoka Tsh. 3,163/= mwezi uliopita, huku mafuta ya Dizeli yakiwa ni Tsh.3,210/= yakiwa yamepanda kutoka Tsh. 3,126/= mwezi uliopita.
.
EWURA imesema kupanda kwa bei hizo, kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za mafuta yaliyosafishwa (FOB), katika soko la dunia kwa wastani wa 3.94% kwa mafuta ya petroli na wastani wa 2.34% kwa mafuta ya dizeli.