Back to top

Daraja la Tanzanite lakamilika kwa 100%, kuanza kutumika Feb 01.

30 January 2022
Share

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa ametangaza kukamilika rasmi kwa kwa 100% kwa daraja la Tanzanite lililojengwa juu ya bahari likitokea Aga Khan hadi Osterbay Jijini Dar es salaam ambapo amebainisha kuwa wananchi watalitumia daraja hilo lililogharimu zaidi ya Bilioni 240 bila malipo yoyote na litaanza kutumika rasmi kuanzia Februari 01, 2022.