Back to top

David Alaba athibitisha kuwa na mpango wa kuondoka Bayern Munich.

16 February 2021
Share

Beki David Alaba amethibitisha kuwa anampango wa kuondoka klabuni Bayern Munich mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia klabu hiyo takriban miaka 13.
.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 anatarajiwa kuondoka kama mchezaji huru ambapo atakuwa amemaliza mkataba wake na klabu hiyo ifikapo mwezi June mwaka huu.
.
Hata hivyo klabu ya Real Madrid, Chelsea na Liverpool zimeonesha nia ya kumsajili beki huyo wa kimataifa wa Austria licha ya yeye mwenyewe kuwa kimya mpaka sasa ni klabu gani anatazamia kujiunga nayo baada ya kumalizana na Bayern.