
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA), imesema imekamata zaidi ya kilo 3000, za dawa za kulevya aina ya heroin na methamphetamine.
.
Akitoa taarifa hiyo Kamishna wa Mamlaka hiyo, Aretas Lyimo, amesema kiwango hicho ni kikubwa zaidi kihistoria kuwahi kukamatwa tangu kuanza kwa shughuli za udhibiti wa dawa za kulevya nchini, huku akibainisha kuwa endapo dawa hizo zingeachwa na kuingia mtaani zingeathiri idadi ya Watanzania zaidi ya Milioni 70.
.
Kamishna huyo amesema kukamatwa kwa dawa hizo ni kutokana na operesheni maalumu iliyofanyika katika mikoa ya Dar es Salaam na Iringa kati ya Disemba 5 hadi 23, 2023, na kwamba watu saba wamekamatwa wakihusika na dawa hizo ambapo wawili kati yao wana asili ya Asia.
