Back to top

DAWASA: KUTAKUWA NA UPUNGUFU WA MAJI KWA SAA 36

04 March 2024
Share

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), imetangaza kuwa, kuanzia kesho Machi 05, 2024, saa 12 jioni, hadi siku ya Alhamisi Machi 7,2024, kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji kwa baadhi ya maeneo ili kuruhusu maboresho ya msingi katika mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini.
.
Mamlaka hiyo imesema maeneo yatakayoathirika na upungufu huo ni Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Kunduchi, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Madale, Goba, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo Kikuu UDSM, Mwenge, Chuo Kikuu Ardhi, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya Jiji. 
.
Kutokana na matengenezo hayo, DAWASA imewashauri wananchi kuhifadhi maji ya kutosha katika kipindi cha matengenezo.