Back to top

DC MSAFIRI ATAKA WAFUGAJI WANAOMILIKI SILAHA WARIPOTI POLISI

16 June 2022
Share


Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Bi.Sara Msafiri amewataka wafugaji wote wanaomiliki silaha aina ya Bunduki kuripoti polisi kujua uhalali wa silaha hizo mara baada ya kuzuka matukio ya baadhi ya wafugaji wenye nguvu kubwa wanaomiliki silaha ikiwemo bunduki kutumia silaha hizo kuwatishia wakulima, kuwakamata na kuwapeleka maeneo ambayo wanaenda kuwapa adhabu zisizostahili.

"Kuna wafugaji ambao wao wana nguvu kubwa wameweza kuomba vibali vya kumiliki silaha na serikali imewapa vibali hivyo, tukiamini wanaenda kwa ajili ya kuimarisha usalama, lakini matokeo yake wafugaji wale wanatumia silaha ikiwemo Bunduki kuwatishia wakulima, kuwakamata, na kuwapeleka kwenye maeneo ambayo wanaenda kuwapa adhabu zisizostahili"DC Msafiri.

Ametoa kauli hiyo alipofanya ziara katika kijiji cha Kitomondo Halmashauri ya Kibaha mkoa wa Pwani kwa lengo la kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji.

"Kuna serikali ya Kijiji baadhi ya viongozi sio waaminifu, unawakuta kwamba wanapokea wafugaji, ambao wanakuja bila kufuata utaratibu, wakiingia wanaenda kulisha kwenye mashamba ya wananchi lakini kuna wananchi nao ambao nao sio waaminifu, wanawakaribisha wafugaji kinyemela, wanawapa maeneo na wanajenga maboma mwisho wa siku mifugo inaenda kulishwa kwenye mashamba ya wananchi"DC Msafiri.