Back to top

DC Msulwa kutuma timu ya ukaguzi mradi wa maji Kiroka, Morogoro.

18 April 2021
Share

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bwana Bakari Msulwa amesema atatuma timu ya ukaguzi kwenye mradi wa maji Kiroka na miradi mingine wilayani humo, ili kubaini ukusanyaji na matumizi ya fedha za maji zinazo kusanywa kwa wateja.

Pia amemwagiza Wakala wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira Wilaya ya Morogoro, kuhakikisha wanatoa elimu kwa kamati za jumuiya ya watumia maji ili kuongeza wigo wa utunzaji wa miundombinu ya maji.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro ameyasema hayo baada ya kikao cha baadhi ya watumishi wa Wakala wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira pamoja na viongozi wa Kata ya Kiroka.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira Wilaya ya Morogoro, Mhandisi Grace Lymo amesema kwa sasa serikali imepanga kukarabati mradi wa maji Kiroka ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.