Back to top

DC MSUYA AWAONYA VISHOKA WANAOWARUBUNI WAKULIMA DODOMA.

20 November 2023
Share

Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma, Bi.Gift Msuya ameke mea vitendo vya vishoka kununua mazao kwa vipimo visivyo sahihi na kuiagiza   Halmashauri ya Wilaya hiyo kuanzisha vituo vya kuuzia mazao ili kudhibiti vishoka ambao wamekuwa wakiwarubuni wakulima.

Bi.Gift Msuya ametoa maelekezo hayo alipokuwa akifungua kikao cha Wakala wa Vipimo Mkoa wa Dodoma na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kilicholenga kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya vipimo.

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Dodoma, Bw.Karimu Zuberi, amewataka wakulima wilayani humo kuacha kuuza mazao yao holela kwa kutumia Rumbesa.

Nao baadhi ya Madiwani wamesema wamejipanga kwenda kuwaelimisha wananchi kupima mazao yao kwa kutumia mizani ili kutopata hasara.