Back to top

DC Mwaipaya kukomesha Uvuvi Haramu, Mwanga, Moshi na Simanjiro.

14 September 2021
Share

Mkuu wa wilaya ya Mwanga mkaoni Kilimanjaro, Bw.Abdallah Mwaipaya amesema kuna haja ya viongozi wote wa wilaya za Mwanga, Moshi na Simanjiro kushirikiana kimbinu katika kudhibiti uvuvi haramu katika bwawa la nyumba ya Mungu linazozizunguka wilaya hizo.
.
Bwana Mwaipaya ametoa tamko hilo alipozungumza na wananchi wa vijiji vya Handeni na Lang'ata baada ya kupokea kero za wananchi wa vijiji hivyo ukiwemo uvuvi haramu ambao umekithiri hasa upande wa wilaya za moshi na simanjiro.