Back to top

DC Tarime awanyooshea kidole RUWASA, ataka miradi ya maji ikamilike.

26 June 2020
Share

Wakala wa huduma za maji vijijini Mkoa wa Mara (RUWASA) imeagizwa kuhakikisha inakamilisha kwa haraka miradi yote ya maji ili  kuondoa adha ya upatikanaji wa maji vijijini hususani kwa akina mama ambao wanaamka usiku wa manane na kutembea umbali mrefu kupata huduma hiyo huku ikihimizwa kuweka uwazi wa matumizi ya maji na kusoma mapato na matumizi ya fedha zinazotolewa na wananchi.

Maagizo hayo yametolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime,Mhandisi Mtemi Msafiri  wakati akizungumza na wadau  wa maji wilaya ya Tarime ambapo amesema wilaya ya tarime vijijini  bado haijafikia lengo la serikali la upatikanaji wa maji vijijini kwa asilimia 85 na badala yake yanapatikana kwa  asilimia 47.6.

Aidha ametoa wiki moja kwa Meneja wa RUWASA kuhakikisha mradi wa Gamasara  ambao  sasa unamiaka miwili bila kukamilika na kudai haoni sababu ya mradi huo kutokutoa maji hadi sasa.