Back to top

DC wilayani Mtwara ataka mkakati kuongeza vyumba vya madarasa.

26 January 2021
Share

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Dastani Kyobya ameutaka uongozi wa manispaa ya Mtwara Mikindani kuwa na mkakati wa kuongeza vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Naliendele ambayo inawanafunzi zaidi ya elfu moja na miambili.

Kyobya amesema hayo baada ya kutembelea shule ya msingi Naliendele kujionea maendeleo ya shule hiyo ambapo pia amepongeza kutokana na kuwa na ufaulu mzuri katika matokeo ya Darasa la nne na la 7.

Amesema shule hiyo mara nyingi imekuwa ikifanya vizuri kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi kuwa na ufaulu mzuri katika mitiani ya kumaliza darasa la 7 na hivyo wanafunzi wote kuanza kidato cha kwanza.

Amesema idadi ya wanafunzi katika shule hiyo ni kubwa hivyo madarasa yaliyopo hayatoshelezi hivyo ni vyema vyumba vya madarasa vikaongezwa ili kuwa na miundombinu ya kutosha.

Hata hivyo mkuu wa wilaya amekemea tabia ya baadhi ya watoto wanaotoka mapunziko kwa ajili ya kurudi nyumbani kupata chakula na baadhi yao kutorejea tena shuleni, ametaka tabia hiyo kukomeshwa na iwapo kuna wazazi wanaendekeza suala hilo hawana budi kuchukuliwa hatua za kisheria.