Back to top

DCEA & TFS YAKAMATA KILO 54,489.65 ZA DAWA ZA KULEVYA

04 April 2024
Share

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wakala wa misitu (TFS) imefanya operesheni katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Iringa, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam na kufanikiwa kukamata jumla ya Kilogramu 54,506.553 za dawa za kulevya za mashambani na viwandani pamoja na kuteketeza ekari 262 za mashamba ya bangi.

Dawa zilizokamatwa ni bangi kilo 54,489.65, mirungi Kilogramu 10.3, heroin gramu 90.93, cocaine gramu 1.98 na Kilogramu 4.623 za aina mpya ya dawa ya kulevya inayoitwa methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) iliyokamatwa jijini Dar es Salaam ikisafirishwa na raia wa Comoro anayeitwa Ahmed Bakar Abdou (32). Watuhumiwa 72 wamekamatwa kuhusika na dawa hizo na baadhi yao tayari wamefikishwa mahakamani.

Methylene dioxy pyrovalerone (MDPV) ni dawa mpya ya kulevya iliyo katika kundi la vichangamshi inayotengenezwa kwa kutumia kemikali bashirifu. Dawa hii ina kemikali inayoweza kuleta madhara ya haraka kwa mtumiaji ikilinganishwa na dawa nyingine za kulevya. Pia, imeongezwa nguvu ya kilevi inayozidi cocaine, heroin na methamphetamine.